Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye
amesema Kuwa ametiwa mbaroni na polisi mara nne kwa muda wa siku sita kufuatia
uchaguzi uliofanyika nchini humo wiki iliyopita. Matokeo ya uchaguzi huo
yalimpa ushindi Rais Yoweri Museven kutawala nchi hiyo kwa muhula wa tano.
Bwana Besigye ambaye yupo kizuizini nyumbani kwake
ameeleza jinsi alivyokamatwa na polisi.
"nilikamatwa na polisi nikiwa nyumbani mwendo
wa saa kumi na moja alfajiri, na kupelekwa kwa mwendo kasi mjini ambao ulikuwa
ni mwendo wa kutisha ili kuwakwepa waandishi wa habari waliokuwepo katika eneo
walinikamata, na hii ilkawa ni mara ya nne kukamatwa na polisi kwa muda wa siku
sita."
Besigye amesema amesikitishwa sana kwamba jamii ya
kimataifa haijaingilia kati suala hilo kwa niaba yake.
Ameonya kwamba kama wanadhani Rais Museveni ameleta
amani na utulivu nchini Uganda wajue wanafanya makosa.
"Amani na utulivu ni upande mmoja wa
sarafu.
Upande wa pili wa sarafu ni haki. Hauwezi kuwa na
amani na utulivu bila haki. Na hii ndio hali halisi katika mazingira yetu ni
kwamba kwa kifupi hakuna haki "alieleza
0 comments:
Post a Comment