WADAIWA 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari
Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na
kufilisiwa.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya
Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao
wamekamilisha malipo, Yono Kevella alisema hayo Dar es Salaam jana.
Akizungumza na gazeti hili, Kevela alisema kuanzia
leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa kukamata na kufilisi mali
za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Kevela alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa,
linazowazuia kutekeleza wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo
alisema, wengi wa wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha
moyo wa kulipa.
Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni Alitaja wadaiwa 16
ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao watafilisiwa wasipojitokeza
kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh 28,249,352.50, Strauss International
(45,393,769.95), Farid Abdallah Salum (52,185, 614.97).
Wengine ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo
Yona Kimaro (64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem
Abdul (130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading
Co.Ltd (448,690,271.90).
Pia wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff
Tyres General Co Ltd, (7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe
(34,687,165.00), Rushwheel Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad
Hamdan (68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah
Salem Sh 75,334,871. 85.
Akizungumzia wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14
walizopewa na zikaisha juzi, alisema wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza
kulipa madeni baada ya kampuni yake kuwafuatilia.
Kevela alisema hadi jana zaidi ya Sh milioni 200
zimelipwa na wadaiwa hao.
Wadaiwa hao 24 walishindwa kulipa kodi kwa wakati
kama walivyotakiwa kufanya, ndipo TRA ilimpa dalali huyo kazi ya kuwafilisi.
Kampuni hiyo ya udalali ilitoa siku 14, kuanzia Februari 10, mwaka huu wawe
wamekamilisha; muda ambao umeisha juzi.
Kevela alisema katika siku hizo 14, kati
waliojitokeza kulipa,wanne kati yao wamemaliza madeni na wengine wanne
wamepunguza madeni na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki. Waliomaliza madeni
yao Wadaiwa waliolipa madeni yao yote ni Issa Ali Salim aliyekuwa akidaiwa Sh
94,543,161.96, Libas Fashion (26,593,245.78), Omary Hussein Badawy (21,346,615.40)
na Zulea Abas Ali (16,760577.24).
Waliopunguza madeni yao Waliopunguza madeni yao ni
Zuleha Abbas Alli aliyelipa Sh milioni 47 na kubakiwa na deni la Sh 28,508,551,
awali alikuwa akidaiwa Sh 75,508,551.88, mwingine ni Ally Awes Hamdani
aliyelipa Sh milioni 17.26 awali alikuwa akidaiwa Sh 55,485,904.07).
Wengine waliopunguza kidogo ni Tifo Global Trading
Co Ltd waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 1,573,300,644.58, Lotai
Steel Tanzania Ltd, waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 5,476,475,738.19.
“Tulikabidhiwa wadaiwa 24 na TRA, waliokwepa kodi
kwa kutorosha kontena katika bandari kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa
walipewa muda wa kulipa ila walikaidi, tukakabidhiwa tuwafilisi mali zao zote
ili kulipia madeni na wamejitokeza hao na kuanza kulipa wengine wamemaliza”,
alisema Kevela.
Awali wadaiwa 24, walikwepa kodi ya Sh bilioni 18.95
kwa kutorosha makontena 329 ya bidhaa zao kutoka Kampuni ya SSB ambayo ndiyo
mmiliki wa bandari kavu ya (Azam ICD) na kampuni ya Regional Cargo Services.
Mapema Desemba mwaka jana aliyekuwa Kaimu Kamishna
wa TRA, Dk Philip Mpango alizungumza na waandishi wa habari na kusema kampuni
15 kati ya 43, zilizokwepa kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya
Azam, wamelipa.
Dk Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo
ilikuwa siku ya mwisho aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa
kodi hao 43, kulipa wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo
wake. Kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na
waliobaki hawakujitokeza kulipa.
0 comments:
Post a Comment