Ugiriki imetishia kupinga maamuzi yote katika
mkutano ujao wa viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu uhamiaji iwapo nchi wanachama
hazitakubaliana kugawana kwa uwiano wahamiaji na wakimbizi.
Hatua hiyo imekuja wakati Austria na baadhi nchi za
Balkani kutoa wito kupunguzwa kwa wahamiaji wanaovuka mipaka ya nchi zao.
Akihutubia bunge mjini Athens Waziri Mkuu wa Ugiriki
Alexis Tsipras amesema haikubaliki kwamba nchi yake iachiwe kukabiliana na
tattizo hilo pekee yake.
"tunachokataa kufanya ni kukubali mabadiliko
katika nchi yetu kuwa ghala kubwa la nafsi za watu , na wakati huo huo
tuendelee kuchukua hatua ndani ya Umoja wa Ulaya na katika mikutano ya viongozi
wa Umoja huo kana kwamba hakuna jambo lolote baya. Kuanzia sasa na kuendelea
Ugiriki haitakubalina na makubaliano kama hatutahakikishiwa mgawanyo wa uwiano
wa mzigo na wajibu wa makazi ya wakimbizi miongoni wa nchi wanachama."
Wakati huo huo mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi 28
za Umoja wa Ulaya zinakutana mjini Brussels asubuhi hii kuzunguzia suala la
tatizo la wakimbizi huku onyo likitolewa kama tatizo hilo litaendelea itakuwa
vigumu kulishughulikia.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kufanya
mikutano miwili kuhusu suala la wahamiaji mwezi ujao ili kujaribu kuwa na sera
kabla wimbi jingine la wahamiaji.
0 comments:
Post a Comment