Idara ya uhamiaji mkoani Morogoro imefanikiwa kuwatia
nguvuni vinara wanne wanaojihusisha na mtandao wa kuingiza na kusafirisha
wahamiaji haramu kutoka nchi mbalimbali duniani kuwapitisha katika mipaka ya
Tanzania kwenda nchi za jirani.
Akitoa tarifa ya kukamatwa kwa mtandao huo naibu kamishina
uhamiaji mkoa wa Morogoro Joseph Malumbu amesema watu hao wamekamatwa na
maafisa uhamiaji kwa nyakati na maeneo tofauti ambapo amesema idara hiyo
haitawavumilia maafisa na vigogo wa serikali wanaojihusisha na mtandao huo na
kwamba watakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.
Aidha naibu kamishina malumbu amewaomba maafisa wa uhamiaji
wa mikoa ya mipakani kutoa ushirikiano wa kutosha na kufanya kazi kwa uadilifu
ili kuahakikisha matukio ya uingizaji na usafirishaji wa wahamiaji haramu
yanakomeshwa.
Mrakibu msaidizi wa uhamiaji mkoa wa Morogoro Juma Kalunga
ametaja majina ya watuhumiwa hao na kueleza namna walivyokamatwa watu hao ndani
ya kipndi cha wiki mbili katika mikoa ya Dar es Salam na Tanga huku wakazi wa
mkoa wa Morogoro wakipongeza jitihada zinazo fanywa na jeshi hilo.
0 comments:
Post a Comment