Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP
Bw Achim Steiner amesema mkutano wa pili kuhusu mazingira utakaoandaliwa na
shirika hilo utafanyika mwezi Mei mjini Nairobi Kenya.
Mkutano huo utahusu kuhimiza ajenda ya uzalishaji usio na
uchafuzi kwa mazingira, kuendana na malengo ya maendeleo endelevu na
makubaliano ya Paris kuhusu kukabiliana na hali ya hewa.
Bw Steiner amesema mkutano huo utatoa fursa kwa wadau
mbalimbali kujadiliana kuhusu mustakbali wa siku za baadaye wenye neema,
shirikishi na wenye mazingira ya asili yanayofaa. Wawakilishi kutoka serikali,
mashirika ya kimataifa, sekta binafsi na jumuiya zisizo za kiserikali
watajadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujangili, uchafuzi wa bahari na
taka za kemikali.
0 comments:
Post a Comment