Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amewafuta kazi takriban
watu ishirini na sita ambao ni wakuu wa idara mbali mbali za serikali ikiwemo
vyombo vya habari.Maafisa hao wametakiwa kukabidhi madaraka kwa maafisa wa
ngazi za juu katika idara zao mpaka kutakapofanywa uteuzi mwengine.
Huu ni mwanzo wa mabadiliko makubwa ambayo yanatarajiwa
kuathiri zaidi ya mamia ya idara za serikali.
Rais Buhari amepata shinikizo kubwa la kufanya mabadiliko
hayo ambayo yangewaachisha kazi maafisa wengi ambao walikuwa karibu na
aliyekuwa rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan. Nafasi zao zinatakiwa
zichukuliwe na wafuasi kutoka chama cha APC, hasa wale waliokuwa na mchango
mkubwa katika uchaguzi uliomwingiza madarakani rais Buhari.
Uteuzi wa nafasi hizo unaonekana kama ni bakshish kwa wale
waliotumia nguvu zao kukiingiza chama madarakani.Inasemekana, wale waliopewa
nafasi hizo mwanzoni, walizitumia kwa manufaa yao binafsi.
Lakini kutokana na ari aliyokuwa nayo rais Buhari ya
kupambana na ufisadi, maafisa hao watakaoteuliwa watakuwa na wakati mgumu.
0 comments:
Post a Comment