Tasnia ya Bongo Flava nchini Tanzania imepata pigo kufuatia
kifo cha Mwanamuziki wa miondoko ya Bongo Flava nchini Tanzania John Woka kufariki
dunia hivi leo jijini Dar es Salaam.
Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema
walipigiwa simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa Michael Denis
aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa jina la Joni Woka amefariki katika hospitali
ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.
Michael Denis a.k.a Joni Woka alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa garage maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani,
Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.
Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal ,Hodi Mganga na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.

Hii ni moja ya kazi za Marehemu John Woka enzi za uhai
wake,Tangulia sisi twaja
0 comments:
Post a Comment