Muigizaji wa Bongo Movie nchini Tanzania Ray Kigosi amesema
kuwa kutokana na mapokeo juu ya unywaji maji na kuwa mweupe anampango ambao
anatarajia kutengeneza makala(Documentary)juu ya umuhimu wa maji.
Akizungumza wakati wa mahojiano yake na kituo kikubwa cha
radio nchini Tanzania Ray amesema hayo na kusema kuwa baada ya suala hilo la
unywaji maji na kuwa mweupe kuwa na kasi kila kona kwake yeye inamuongezea kitu
flani kwani hata kampuni za uzalishaji maji zinaweza kumtumia.
Amesema ingekuwa nje ya Tanzania ingekuwa ni rahisi kwa
aidia hiyo kuchukuliwa na hivyo kuangaliwa Product mbalimbali juu ya umuhimu wa
maji kwa mwanadamu.
Hivi karibuni katika baadhi ya mitandao ya kijamii Ray
amekuwa gumzo hadi sasa baada ya kuhojiwa kupitia Radio Clouds juu ya weupe wake
na kusema kuwa kinachofanya hivyo ni kufanya mazoezi na kunywa maji kwa
wingi,jambo ambalo limechukuliwa tofauti na jamii na kuona kuwa huenda kuwa
hakuna ukweli juu ya hilo.
Badhi ya picha ambazo zimekuwa zikisambaa kupitia mitandao
ya kijamii haswa kwenye mtandao wa Whatsapp zimekuwa zikionesha watu wakinywa
maji kwa wingi kwa kutumia madumu makubwa na wengine kunywa visimani kama
ng”ombe kusudi waone ninamna gani maji yanasaidia kubadilisha rangi ya mwili na
kuwa mweupe.
Haya ni Mahojiano yanayokukumbusha alichokisema juu ya weupe
wake kabla ya kuzua gumzo.
0 comments:
Post a Comment