RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Af rika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi Ia Polisi
na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,
imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dk. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mathias
Meinrad Chikawe na Dk. Ramadhan Dau na kwamba, vituo vya uwakilishi kwa mabalozi
hao vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.
Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja
walioteuliwa kuwa ni Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Nyakoro Sirro ambaye
amepandishwa cheo na kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuwa Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa
wazi na Kamishna Mstaafu, Suleiman Kova.
Albert Nyamuhanga, Naibu Kamishna wa Polisi ambaye
amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya
Fedha, Utawala na Lojistiki.
Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na
Kamishna wa Polisi, Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Mwanza.
Naibu Kamishna wa Polisi, Robert Boaz Mikomangwa ambaye
amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya
Intelijensia.
Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na
Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
0 comments:
Post a Comment