Image
Image

Matengenezo ya kivuko cha MV Kilombero II yakamilika.




Matengenezo ya kivuko cha  Mto Kilombero,MV Kilombero II yamekamilika na kivuko hicho kimeingizwa rasmi majini baada ya kupinduka na kusababisha watu wawili  kufariki dunia na wengine 35 kunusurika  tarehe 27  mwezi uliopita .
Meneja Mfuatiliaji wa Vivuko na Meli ,  kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd ya Mwanza, HEMED KARONZO amesema baada ya kuk iibua na kukitoa nchi kavu,walik ifanyia matengenezo ya jumla kivuko hicho ikiwemo kuziba matundu chini ya kifua cha kivuko  kuanzia tarehe  10 hadi  jana  kilipokamilika na kukiingiz w a majini majira ya mchana.
Amesema kazi nyingine zilizofanyika ni kuweka milango ya kutokea magari na abiria, kupaka rangi, kutengeneza mifumo ya umeme, kujenga vibanda vya kupumzikia abiria na viti vyake na bomba za kingo za kivuko .
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme,MAGRETH MAPELA ameeleza kuwa baada ya kivuko kuingizwa majini,   marekebisho madogo madogo ikiwemo mifumo ya umeme na usukani vitaf anywa na hatimaye wawashe injini  kwa majaribio ya awali,   kabla ya mengine yatakayofanywa na Mamlaka ya Huduma za Usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment