Serikali ya Tanzania ya awamu ya tano imesema kuwa
bado itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi hadi itakapo
jiridhisha kwamba vitendo hivyo vimekwisha na nchi inakwenda katika mstari
ulionyooka ili kuweka usawa kwa walionacho na wasio nacho.
Kauli hiyo ameitoa Waziri mkuu Kassim Majaliwa
wakati alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya maadili kwa mawaziri
na manaibu waziri jijini Dar es Salaam.
Mhe.Majaliwa amesema vitendo vya rushwa na ufisadi
vinatia hasara serikali ya mamilioni ya fedha ambazo zingeweza kutumika
kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi na kusisitiza
tatizo hilo linaweza kupungua iwapo viongozi watazingatia sheria ya maadili.
0 comments:
Post a Comment