Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud ametoa
maelezo kuhusu idadi ya wanajeshi wa Kenya waliofariki kufuatia shambulio la
al-Shabab katika kambi yao huko el-Adde mwezi uliopita.
Rais huyo ametoa idadi hiyo kuwa kati ya wanajeshi
180 na 200 katika mahojiano na runinga moja ya Somali Cable TV.
Wapiganaji hao wa al-Shabab wamesema kuwa wanajeshi
100 walifariki.Kenya haijatoa idadi yoyote ya wanajeshi wake waliofariki
kufikia sasa.
Rais huyo wa Somalia alikuwa akitetea ziara yake
nchini Kenya baada ya hisia kali kutolewa katika mitandao ya kijamii kufuatia
shambulio la mgahawa wa Lido Beach katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu mnamo
mwezi Januari.
Alisema kuwa ilikuwa muhimu kutoa heshima kwa
wanajeshi wa Kenya waliouawa:.
''Wanajeshi wa kigeni hufariki na hatuendi katika
mazishi yao.wakati wanajeshi 180 ama 200 wa kenya waliotumwa nchini Somalia na
sabab ya kutumwa kwao nchini humo ni kuleta udhabiti kuwaisaidia raia wa
Somalia na wanauawa alfajiri moja ,si swala la kawaida kwamba wageni
wameuawa.Kile kilichosalia ni kwamba jamaa zao walielezwa kwamba kulikuwa na
vita na watu wao wakafariki kutokana na hilo'',alisema Sheikh Hassan Mahmoud.
BBC imewasiliana na maafisa wa jeshi la Kenya ambao
bado hawajazungumzia habari hizi.
Baada ya shambulio hilo kutokea tarehe 15
Januari, Rais Kenyatta aliahidi kwamba majeshi ya Kenya yangewaandama
waliohusika.
0 comments:
Post a Comment