Baada ya muda mchache Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli kutoa Agizo kwa mawaziri ambao hawajajaza
Tamko la Rasilimali na Madeni wawe wamejaza fomu hizo na kuzirejesha katika
Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam ifikapo leo
saa 12.00 jioni hatimaye limeanza kutekelezwa.
Kutekelezwa huko kumekuja Baada ya waziri mkuu
kutaja majina ya mawaziri wanne na naibu waziri mmoja ambao hawajarudhisha fomu
za Sekretariati ya maadili ya umma na kutakiwa wawe wamerejesha fomu hizo
leo
Baada ya agizo hilo sasa aliyerudisha fomu hizo ni
waziri wa mambo ya nje,ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Mhe.Balozi Dkt.Augustine Mahiga ambapo amekiri kuwa ni kweli alikuwa
hajarudisha fomu hizo kutokana na majukumu ya kazi yaliyokuwa yamembana
Baada ya zoezi hilo kutolewa muda wa kurudisha na
Rais Magufuli waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga ambaye naye ametajwa
kutorudisha fomu hizo ameonekana kushangazwa na jina lake likitajwa wakati
ameshazirudisha na kwa sasa ameelekea ofisi za Sektretariati ya maadili
kuwasilisha malalamiko yake.
Katika hatua nyingine naibu waziri wa ofisi ya
makamu wa rais,Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina amesema kuwa atawahisha
kurudisha fomu hizo kabla ya saa kumi na mbili jioni.
0 comments:
Post a Comment