Image
Image

Maziko ya Marehemu Mapili kufanyika Makaburi ya kisutu Leo.


Mwanamuziki nguli wa muziki wa Dance nchini Tanzania Mzee Kassim  Mapili (Pichani kulia) aliyefariki dunia alipokuwa yupo Chumbani kwake Tabata kwa Muda Mrefu anatarajiwa kuzikwa leo Makaburi ya kisutu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ratiba ya Msiba wa Marehemu Mapili upo Magomeni Mapipa nyumba No.20. na Maziko yatafanyika mwendo wa Saa kumi katika makaburi ya kisutu jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizokuwa zimepatikana juu ya kifo cha mzee Mapili nikuwa toka siku tatu nyuma hakuonekana jambo ambalo lilistua wengi ndipo kufika anamoishi ikabidi kuvujwa mlango na kukutwa ndani akiwa
Mara ya mwisho hadharani Marehemu Mzee Kassim Mapili alionekana akiongoza wanamuziki katika mazishi ya mwanahabari nguli wa burudani Marehemu Fred Mosha katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, ambako pamoja na kushirki mazishi aliimba kwa hisia beti kadhaa za kumuenzi marehemu Fred.
Marehemu mzee Kassim Mapili Enzi za uhai wake amekuwa ni mpiga gitaa Mahiri ambae alipigia Bendi ya Polisi Jazz wana Vangavanga.
Lakini Mzee Mapili hakutunga wala kushiriki wimbo wa Nipate lau nafasi kwani wimbo huu aliutunga Marehem Ahmed Kipande akiwa na kundi la Kilwa Jazz mwaka 1967 na ile sauti inayoimba ni Ahmed Kipande.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment