Rais Obama amepanga kuchukua hatua ya kumaliza
uhasama unaondelea nchini Syria kwa kuwapa onyo vyama vyote vinavyohusika na
mgogoro ambao unaangaliwa na dunia na kama wataweza kutimiza ahadi zao.
Taarifa zilizokuja usiku wa kuamkia Leo,zinasema
raisi Obama amechukua hatua madhubuti ili kumaliza mgogoro huo.Amesema mgogoro
ambao upo kati ya waasi pamoja na kampeni baina ya kikundi cha kigaidi cha
wanamgambo wa kiislamu wa IS una maana kuwa mwisho mwa mgogoro huo hautaweza
kuisha kwa haraka.
Lakini raisi huyo amesisitiza pia kuwa hiyo ni fursa
ya kuweza kuwa na maongezi ya amani.
Wanaharakati wanasema waasi wanakumbana na
mashambulizi makali ya anga kaskazini mwa jimbo la Latakia na kwa waasi waliopo
karibu na Damascus.
0 comments:
Post a Comment