Image
Image

Uchaguzi ya Iran vituo 1062 VINATUMIKA KWA ajili ya uchaguzi wa leo wa Bunge.

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Iran amesema kuwa maandalizi na taratibu zote za uchaguzi wa kumi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na wa tano Baraza la Wataalamu zimekamilika.

Muhammad Hussein Muqimi amesema vituo 1062 vimeyatarishwa kote nchini kwa ajili ya uchaguzi wa leo wa Bunge la Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi wa Juu wa Iran. Amesema kuwa nyezo na vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kupiga kura vimepelekwa mapema katika majimbo yote ya uchaguzi hapa nchini.
Muqimi ameongeza kuwa uchaguzi huo umeanza asubuhi hii saa mbili kamili na utaendelea kwa masaa kumi hadi saa 12 jioni. Amesisitiza kuwa muda huo yumkini ukazidishwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura iwapo italazimu.
Karibu Wairani milioni 55 wametimiza masharti ya kupiga kura katika chaguzi hizo mbili.
Waandishi habari 473 kutoka nchi 29 duniani wapo hapa nchini kwa ajili ya kuripoti matukio ya uchaguzi wa leo.
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu pia amewataka wananchi wote waliotimzia masharti kushiriki kwa wingi na kwa nishati katika zoezi hilo la kidemokrasia ili kuzidisha nguvu ya taifa na rasilimali ya kijamii ya Iran kwa kuonesha umoja na maadili ya Kiislamu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment