Aliyekuwa mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose
Mourinho amesema kuwa hajui iwapo atakuwa mkufunzi wa kilabu ya Manchester
United lakini anatumai kwamba atapata ajira ya kuifunza kilabu nyengine
mwishoni mwa msimu huu.
Mapema mwezi huu BBC iliripoti kwamba Mourinho
amekutana na maafisa wa kilabu ya Manchester United.
Mourinho mwenye umri wa miaka 53 alifutwa kazi mnamo
mwezi Disemba,miezi saba baada ya kushinda kombe la ligi kuu nchini Uingereza.
Na alipoulizwa iwapo atachukua mahala pake Luis Van
Gaal katika uwanja wa Old Trafford,Mourinho alijibu: ''hilo ni swali kubwa
sana''.
Akizungumza katika shule moja nchini
Singapore,aliongeza:Hakuna mtu anayejua na mimi ni wa kwanza kutojua,nasoma
kuhusu mambo mengi tofauti.Ninaangalia siku za usoni na shauku nyingi.Kwa sasa
nafurahia maisha yangu ya faragha wakati huu ambao siko kazini na natumai
kwamba nitarudi mwishoni mwa msimu huu.Iwapo nataka kurudi kesho nitarudi
kesho.Nadhani ni muhimu kusubiri badala ya kukimbiliajambo.
Nitaanza msimu ujao na kilabu mpya na mradi huo
nadhani ni mzuri sana kwangu mimi.
Manchester United ni ya tano katika ligi ya
Uingereza,ikiwa iko alama sita nyuma ya Kilabu ya Manchester City ambayo iko
katika nafasi ya tano.
0 comments:
Post a Comment