Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya imeendelea
tena usiku wa Jumatano kwa michezo miwili , Ambapo Klabu ya soka ya Manchester
city imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa magoli 3-1 dhidi ya Dynamo Kiev
.
Magoli ya Manchester city katika mchezo huo
yamefungwa na wachezaji Sergio Aguero dk15 , David Silva dk 40, huku bao la
tatu likifungwa na Yahya Touré dk 90.
Kwa upande wa Dynamo Kiev bao lao la kufutia machozi
limefungwa na Vital Buyal-sky dk 58
Katika mchezo mwingine Psv Eindhovein wakiwa
nyumbani wametoshana nguvu na Atletico Madrid kufuatia sare tasa ya bila
kufungana.
Michuano hiyo itaendelea tena March 8, 2016 kwa
mechi mbili ambapo Real Madrid itaikaribisha Fc Roma na VfL Wolf- Sburg
ikichuana na KAA Gent.
0 comments:
Post a Comment