Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van
Gaal amewataka wachezaji wake kuwa na ''uchu'' katika mechi ya kombe la Europa
dhidi ya FC Midtylland.
United iko nyuma kwa mabao 2-1 na itaikaribisha timu
hiyo ya Denmark nyumbani.
Na alipulizwa kile alichokihitaji kutoka kwa timu
yake ,Van Gaal alijibu: Tamaa,njaa mara nyingi mimi hutumia neno ''uchu''.
Ufanisi katika ligi ya Europa ndio matumaini makubwa
ya Manchester United kufuzu katika ligi ya vilabu bingwa Ulaya.
Baada ya kupoteza 2-1 kwa Sunderland katika ligi ya
Uingereza,mashetani hao wekundu wana alama sita chini ya kilabu ya nne katika
jedwali la ligi ya Uingereza.
Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 64 anakabiliwa na
madai kwamba huenda kazi yake ikachukuliwa na aliyekuwa mkufunzi wa Manchester
United Jose Mourinho na amekuwa akikosolewa na mashabiki.
0 comments:
Post a Comment