Mvulana wa taifa la Afghanistan ambaye aligonga
vichwa vya mitandao ya kijamii alipovaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na
jina la Lionel Messi hatimaye amepata jezi nzuri kutoka kwa mshambuliaji huyo
wa Argentina.
BBC ilimsaidia Messi kumtafuta mtoto huyo ambaye
anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo wa Argentina.
Murtaza Ahmadi mwenye umri wa miaka 5, anatoka
katika wilaya ya Jaghori mashariki mwa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.
Timu ya usimamizi wa Messi ilithibitisha siku ya
Alhamisi kwamba Murtaza alitumiwa jezi ya mshambuliaji huyo wa Argentina
iliotiwa saini pamoja na mpira kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona ambaye
ametuzwa kuwa mchezaji bora mara tano.
''Ninampnda Messi na fulana yangu inasema Messi
ananipenda,Murtaza alisema,tayari akimuigiza mshambuliaji huyo anavyosheherekea
bao lake.
Msako wa mtoto huyo katika mtandao ulisababishwa na
picha moja ilioenea katika mitandao ikimuonyesha amevaa fulana ya plastiki ya
Messi.
Madai baadaye yalizuka kwamba mvulana huyo ni
wa Kikurdi kutoka Iraq na kwamba nyota huyo wa Barcelona alitaka kumtafuta na
kumpa jezi nzuri.
0 comments:
Post a Comment