Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi OSHA
wametakiwa kufuatilia kwa karibu maeneo ya wachimbaji wadogo ambao maisha yao
yapo hatarini kutokana na kutozingatiwa kwa kanuni za usalama na afya na hivyo
kuhatarisha maisha ya wachimbaji.
Mkoa wa Geita wakazi wake wamejikita katika
uchimbaji ambapo baadhi ya Kampuni ndogo za uchimbaji zimekuwa zikiwatumikisha
wafanyakazi wao kuchenjua dhahabu kwa kutumia sumu ya zebaki wakiwa hawana
vifaa na usalama wao ni mdogo.
Bado kuna changamoto nyingi kwa wafanyakazi,
ikiwemo kupata madhara kwa kutumia kemikali lakini hakuna hatua za makusudi
zinazochukuliwa kwa waathirika waliopata madhara hayo.
Mtendaji Mkuu OSHA Akwilima Kayumba amesema Osha
imetoa elimu kwa wachimbaji wadogo na wakubwa pamoja na wajasiriamali ili kila
mmoja atimize wajibu wake mahala pa kazi ili kuleta tija katika uzalishaji.
Wadau wengi akiwemo Meneja Usalama Kasco
Construction Balthazar Madaha wanaona kuna haja OSHA kufika maeneo ya
uchimbaji ambapo ndio kuna maisha ya vijana na wanaozunguka maeneo hayo kuwa
hatarini.
Mtendaji Mkuu OSHA Akwilima Kayumba amesema OSHA ina
lengo la kuhakikisha usalama mahala pa kazi na na leseni ya osha inatolewa bure
ikiwa umetimiza vigezo.
Hata hivyo Wafanyakazi wametakiwa kuwezeshwe
kuunda matawi ya wafanyakazi na kupewe mafunzo juu ya usalama mahali pa kazi
pamoja na kuwa na kamati za afya ambazo zitashiriki katika matumizi salama ya
kemikali.
0 comments:
Post a Comment