POLISI mkoani Morogoro inawashikilia wahamiaji
haramu 12 raia wa nchini Ethiopia waliokamatwa katika eneo la Mikumi wilayani
Kilosa wakiwa safarini kuelekea Tunduma kwaajili ya kuvuka kwenda nchini Afrika
ya Kusini.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard
Paulo amesema kuwa wahamiaji hao wamekamatwa na askari waliokuwa doria majira
ya saa 8:30 usiku katika eneo la Mikumi kwenye barabara ya kuu ya
Morogoro-Iringa.
Amesema wahamiaji hao haramu wamekamatwa kwenye gari
lenye namba za usajili T 786 BHZ aina ya Toyota Noah, lililokuwa likiendeshwa
na Hakimu Mustafa akiwa na kondakta wake Rashidi Ally wote wakazi wa Segera
mkoani Tanga.
Waliokamatwa ni Ndita Pundas (18), Emasige Tasama
(21), shadio Jamali (18), Belei Kitacho (20), Daniel Abro (22), Wondim Alficha
(22), Ashenaac Malesa (23), Azra Lathim (18), Dawiti Petrosi (20), Daudi Havarc
(30), Noerej Daniel (19) na Mhari Samli (30) na katika mahojiano ya awali
wamedai wanaishi katika mji wa Addis Ababa nchini Ethiopia.
Aidha Paul amesema kuwa wanaendelea kufuatilia
majina na watu waliohusika kupanga njama za kusafirishwa kwa wahamiaji hao
haramu ili hatua za kisheria zifuatwe na kwamba Dereva wa gari hilo Hakimu
Mustafa amedai akiwa Segera Tanga alipigiwa simu na mhusika wa gari hilo
akimtaka akafuate abiria kuwatoa Chalinze kuwapeleka Tunduma bila kufahamu ni
watu wa gani.
Hata hivyo kamanda huyo wa Polisi amewaonya wananchi
kujihusisha na biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu na kwamba Jeshi hilo
limejipanga kukabiliana na wahamiaji hao na wanaowasafirisha kwa kuwachukulia
hatua kwa mujibu wa sheria.
0 comments:
Post a Comment