Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de
Maiziere anaefanya ziara nchini Afghanistan ameiahidi nchi hiyo msaada wa fedha
ili iweze kuwagharimia wakimbizi wanaorejea kutoka Ujerumani.
Waziri de Maiziere pia amesema wanajeshi wa
Ujerumani wataendelea kulinda usalama nchini humo. Waziri de Maiziere
aliewasili nchini Afghanistan wakati ambapo magaidi walifanya mashambulio na
kuua watu zaidi ya 20 amewataka vijana wabakie nyumbani ili waijenge nchi yao.
Ujumbe wazi ninaotaka kuuwailisha ni kwamba
tutaendelea kuwapo nchini Afghanistan.Na kwa upande wetu matarajio ya wazi
tuliyonayo juu watu wa Afghanistan ni kwamba mtabakia hapa ili muijenge
nchi"
Wakati waziri de Maiziere ametilia maanani kwamba
hali ya usalama ni ya kutatanisha nchini Afghanistan, ameeleza kuwa idadi kubwa
ya watu wa nchi hiyo hawaendi Ujerumani kwa sababu ya hali mbaya ya usalama ,
bali amesema watu hao wanavutiwa na hali ya bora ya maisha nchini Ujerumani:
Wakimbizi wa Kiafghanistan wakifanya maandamano
Köln, Ujerumani
Ni wazi kwamba hali ya usalama nchini Afghanistan ni
ya kutatanisha na hakuna anaekanusha hayo.
Ndiyo sababu kwamba wanajeshi kutoka nchi za nje
wapo hapa kwa ajili ya kuiunga mkono serikali.Hata hivyo hali inatafautiana.
Aghalabu ni mashambulio yanayoripotiwa zaidi kuliko yale yanayozuiliwa. Magaidi
wanawatishia watu wote duniani na siyo wa Afghanistan tu.
Ndiyo sababu mtu hapaswi kutetereka katika sera
zake"
Hapo jana tu magaidi walifanya mashambulio mengine
katika mji wa Kabul na kuwaua watu zaidi ya 10 na kuwajeruhi wengine zaidi ya
20.
Kutokana na hali hiyo waziri huyo wa Ujerumani
amesema wanajeshi wa Ujerumani 850 wataendelea kuwapo nchini Afghanistan kwa
kadri itakavyoendelea kuwa lazima.
Askari hao wapo nchini humo kama sehemu ya jeshi la
kimataifa la NATO linalolinda amani.
Maalfu ya raia na wanajeshi wa Afghanistan waliuawa
mwaka uliopita.
Na kutokana na hali hiyo Waziri de Maiziere amesema
ushirikiano baina ya polisi wa Ujerumani na Afghanistan utaendelezwa.
Lengo la ziara ya Waziri de Maiziere nchini
Afghanistan ni kujadili njia ya kupunguza idadi ya wakimbizi wa nchi hiyo
wanaokimbilia Ujerumani.
Mnamo mwaka uliopita wakimbizi kutoka Afghanistan
walikuwa kundi la pili kwa idadi kubwa. Wakimbizi 150,000 waliokuja Ujerumani
mwaka uliopita walitoka Afganistan.
Kuhusu msaada wa fedha kwa ajili ya Afghanistan
waziri de Maiziere ameeleza kuwa fedha hizo zitapaswa ziekezwe katika miradi ya
miundo mbinu na pia zitumike kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wanaorejea
nyumbani kutoka Ujerumani.Katika ziara yake bwana de Maitziere pia alikutana na
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani.
0 comments:
Post a Comment