SERIKALI imejipanga kuboresha zaidi mpango wa
kunusuru Kaya masikini nchini ujulikanao kama TASAF kwa awamu ya tatu kwa
kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa na kuondoa
malalamiko ya wananchi kuwa mpango huu umekuwa ni wa Kaya chache na fedha hizo
utolewa kwa upendeleo.
Akijibu swali la Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge
wa Kaliua (CUF) lililouliza ni vigezo gani vinatumika kuondoa Kaya
zilizopendekezwa kwenye mradi na kubakiza Kaya chache, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki
amesema mpango wa kunusuru Kaya maskini hutambulishwa kijijini na wataalam
kutoka Halmashauri husika kwa kusimamiwa na uongozi wa kijiji kisha kuweka
vigezo vya Kaya maskini.
“ Wakusanya taarifa huchaguliwa kutoka miongoni mwa
vijana wanaoishi kijijini hapo na kupitia nyumba kwa nyumba kuorodhesha Kaya
ambazo zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na mkutano wa Kijiji ila bado kuna
malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini zinaachwa na kupewa Kaya nyingine
ambazo sio maskini kwa kuliona tatizo hilo suala hili tunalifanyia uchunguzi na
tunaomba watu watoe taarifa ikiwa wataona ukiukwaji wa uorodheshaji wa Kaya
zitakazohusika na mpango huu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya yoyote
atakaye bainika kufanya hivyo”
“ Mpaka sasa kutokana malalamiko yaliyojitokeza
katika kuorodhesha Kaya maskini zinazotakiwa kuwezeshwa na mpango huu
tumewaajibisha watendaji toka Wilaya za Karagwe, Kagera na Kibondo, Kigoma na
tuomba kupewa taarifa kwa sehemu yoyote ambapo kutatokea tatizo kama hili na
tutachukua hatua mara moja kuokoa fedha zilizotakiwa kwenda kusaidia watu
husika” Alisema Mhe Angella Kairuki
Aidha Mhe. Angella Kairuki ameongeza kuwa kuna
taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha za
freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizi zizantolewa na Serikali
ili kusaidia Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata
Elimu Malazi na chakula bora.
TASAF ni mpango wa kunusuru Kaya maskini na imekuwa
katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha Kaya maskini
kujikwamua kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment