Wakati wananchi nchini Uganda waliotimiza masharti ya kupiga
kura leo wakiwa katika vituo vyao vya kupigia kura l;eo kumchagua Rais na
wawakilishi wao wa Bunge dosari zimeanza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuchelewa
kwa vifaa vya kupigia kura na sehemu nyingine kuto kuanza zoezi hilo mapema.
Misururu mirefu ya wapiga kura imejitokeza kushiriki zoezi
hilo licha ya kuwa na upinzani mkubwa na uchaguzi huo ukitajwa na wataalam wa
mambo kuwa una hamasa kubwa mnoo nchini humo.
Inaelezwa kuwa,raia wapatao milioni 15 wa nchi hiyo
waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanamchagua Rais mpya wa nchi hiyo
pamoja na wawakilishi wao wa Bunge lijalo.
Wagombea wanane wanachuana kuwani kiti cha Rais hata hivyo
kati ya wagombea hao wanane ni watatu tu miongoni mwao ndio waliotajwa sana
katika kampeni za uchaguzi huo.
Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani nchini Uganda
tangu mwaka 1986 anachuana na Kizza Besigye mgombea wa chama cha FDC na Amama
Mbabazi aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wake. Uchaguzi wa leo unafanyika huku wapinzani
wakiendelea kulalamika kwamba,serikali ya Rais Museveni imekuwa ikiwabana na
kuwakandamiza wafuasi wao hasa katika kampeni za uchaguzi wa mara hii.
Huku Tume ya Uchaguzi ya Uganda ikisisitiza kwamba,uchaguzi wa
leo utakuwa huru na wa haki,wagombea wa upinzani wameonya kuhusiana na hatua
yoyote ile ya kuiba kura au kufanya udanganyifu.
Amama Mbabazi amesema, hatayakubali matokeo ya uchaguzi huo
endapo itabainika kwamba,kulikuwa na mchezo mchafu wa kuiba kura. Weledi wa
mambo wanasema, kuna uwezekano mkubwa Rais Museveni akashinda tea kiti cha
urais na kuendelea kutawala nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment