Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati)
akimfafanulia jambo Mwekezaji kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini
Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) na Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara
wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), wakati wawekezaji hao
walipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo
kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara
la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi
Swabury, na wapili kushoto ni Mwakilishi wa TPSF ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimsikiliza
Mwekezaji kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje
wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer
(kulia) wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa majukumu mbalimbali
wanayoyafanya katika kampuni yake. Kulia kwake ni Rais wa Klabu ya
Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl. Wawekezaji hao walipomtembelea
Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya
kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya
na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)-(ESSB).
Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na wawekezaji kutoka Bara la Ulaya, ambao ni Mkurugenzi
wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan
Schampheleer (kulia), Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk.
Erick Gohl (wapili kulia), Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Daraja la
Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (Sadc)-(ESSB), Dk. Alawi Swabury, na wapili kushoto ni
Mwakilishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha.
Wawekezaji hao walikutana katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es
Salaam leo.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment