WILAYA ya BABATI mkoani MANYARA, imefanikiwa kudhibiti
ugonjwa wa kipindundu ambapo watu 48 wameugua ugonjwa huo tangu uzuke majuma
kadhaa yaliyopita wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya BABATI CRISPIN MEELA, ametoa taarifa hiyo
wakati akizindua choo cha mfano kilichojengwa kwa ufadhili wa shirika la
Kimataifa la WATER AID katika shule ya msingi DAREDA MISION kwa gharama ya
shilingi milioni 25
MEELA amewataka wakazi wa wilaya hiyo kujenga vyoo na
kuvitumia ili kuepukana na maradhi ya mlipuko.
Aidha ameshukuru Shirika la WATERAID na wahisani wengine kwa
kuanzisha mradi wa kujenga vyoo vya kisasa kwenye baadhi ya shule za msingi
wilayani BABATI.
0 comments:
Post a Comment