Hii ni baada ya polisi katika mji wa Shandong kutangaza mwezi uliopita kwamba wamemkamata mama na bintie wanaoshukiwa kununua na kuuza chanjo kinyume cha sheria.
Chanjo zinazokadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 88 hazikutunzwa kwenye friji kama inavyotakiwa ama kusafirishwa.
Mtandao wa chanjo zisizokubalika unaosemekana kuanza biashara hiyo haramu tangu mwaka 2011, umezusha hasira kali kote nchini Uchina.
Sakata hiyo imesababisha msako mkali, huku ukaguzi ukifanywa miongoni mwa watengenezaji wa chanjo, wauzaji wa jumla na wanunuzi wa bidhaa hiyo.
Chanjo zilinunuliwa kutoka kwa vyanzo mbali mbali , vyenye leseni na vibali na baadae kuuzwa kwa wakala walio halali na wasio halali kisheria pamoja na taasisi za uuzaji na udhibiti wa magonjwa kwa bei rahisi, liliripoti shirika la habari za latafa Xinhua.
0 comments:
Post a Comment