Ugonjwa wa EBOLA unaelekea kurudi kwa kasi nchini
Guinea, kwani idadi ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa sasa wa ugonjwa wa
EBOLA sasa imefikia watu watano.
Idadi hiyo imetolewa na maafisa wa afya
waliokaririwa na mashirika ya habari na zaidi ya watu 800 ambao huenda
waligusana na watu waliokufa wamewekwa chini ya karantini ya wiki tatu
kufuatilia hali yao.
Kufuatia mlipuko huo wa sasa Lberia imefunga sehemu
ya mpaka wake na Guinea.
Katika mlipuko wa kwanza mwaka 2013 zaidi ya watu
11,000 walikufa Guinea, Liberia na Sierra Leone na tangu mlipuko huo uthibitiwe
nchi zote tatu zimeshuhudia milipuko mingine ya hapa na pale.
0 comments:
Post a Comment