Na Raymond Mushumbusi- MAELEZO.
SERIKALI imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini
kuwa Sheria itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto mbalimbali
zinazowakabili kwa sasa.
Waziri Ummy amesema wazee wanakumbwa na changamoto
nyingi katika maisha yao ya kila siku nakusema kuwa azma ya Serikali ya awamu
ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata mahitaji yao muhimu ambayo ni huduma ya
afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.
“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha
kuandikwa kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na kuipeleka katika Bungeni
mwezi Septemba ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi
kutekeleza masuala yahusio wazee” Alisema Mhe.Ummy.
Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee
Hemed Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa
kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara ambayo itawasaidia kutatua changamoto
zinazowakabili na wanaimani na Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya
wazee wa Tanzania waishi katika maisha mazuri.
Aidha Waziri Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri
zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao kuanzisha na kuboresha
madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa huduma kwa wazee ni bure kuanzia
kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha wazee kuungwa kwenye Mfuko
wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya katika maeneo mengi zaidi.
Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa
wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kujadili mshtakabali wa maendeleo ya wazee
nchini.
0 comments:
Post a Comment