Wakulima wa Korosho Wilaya ya Masasi , Kata ya Sindano Mkoani Mtwara wamelazimika
kumuondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha Ushirika cha
Luatala Amcos kwa madai ya kushindwa
kutoa mchanga nuo wa malipo ya tatu ya
korosho kwa wanachama wake.
Wanachama hao wamesema wamelazimika kuchukua hatua baada ya viongozi hao kukaidi agizo la
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara , HALIMA
DENDEGO aliyeviagiza vyama vya ushirika kuhakikisha wanakokotoa bei ya malipo ya korosho na kuzibandika katika ofisi
zao ili wakulima wafahamu mauzo ya korosho yaliyopatikana na kiasi
watakachopata kama malipo ya ziada.
Wamesema pamoja na maagizo hayo ni vyama vichaache
vimefanikiwa kutimiza agizo hilo huku
vyama vingine vikishindwa kufanya hivyo na ku sababisha migogoro baina ya wakulimaa na viongozi wa
vyama vya ushirika.
Wakizungumzia migogoro hiyo watendaji wa Kata ya
Likokona na Chikolopola ,CHARLES JAMES wa Chikolopola na ABASI AKITI wa Kata ya
Likokokona wamesema migogoro hiyo kwa
sasa ni mikubwa baina ya viongozi wa vyama vya ushirika na wakulima na tayari
taarifa hizo zimefika kwa wakuu wa wilaya ambao ni viongozi wa kamati za ulinzi
na usalama ili zifanyiwe kazi.
0 comments:
Post a Comment