Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga waliojilipua
katika uwanja wa ndege wa Brussels Jumanne wametambuliwa kuwa ndugu wawili,
Khalid na Brahim el-Bakraoui.
Kituo cha runinga cha RTBF kimesema wawili hao
walifahamika vyema na polisi.
Mwanamume wa tatu aliyeonekana kwenye video za
kamera za siri uwanja wa ndege akiwa pamoja na wawili hao bado anasakwa.
Milipuko miwili ilitokea katika uwanja wa ndege na
mwingine mmoja katika kituo cha treni na kuua watu 34 na kujeruhi wengine 250.
Ubelgiji imeanza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
RTBF imesema ndugu hao wawili walifahamika na polisi
na wana rekodi za uhalifu lakini hawakudhaniwa kuwa na uhusiano na ugaidi
awali.
Kituo hicho cha runinga kimesema Khalid el-Bakraoui
alitumia jina bandia kukodi nyumba katika eneo la Forest jijini Brussels ambapo
polisi walimuua mtu mwenye silaha kwenye makabiliano wiki iliyopita.
Ilikuwa ni wakati wa msako huo ambapo polisi
walipata alama za vidole za Salah Abdeslam, mshukiwa mkuu wa mashambulio ya
Paris ya 13 Novemba.
Abdesalam alikamatwa kwenye operesheni ya maafisa wa
usalama Ijumaa.
0 comments:
Post a Comment