Watu tisa wamelazwa katika zahanati ya Mpekenyela
wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi baada ya kula samaki wanaosadikiwa kuwa na
vimelea vya ugonjwa wa Kipindupindu na kuwasababishia kuhara na kutapika na kupoteza
nguvu.
Kufuatia tukio hilo wafanyabiashara wawili wa Samaki
katika kata ya Mpekenyela na Namungo wilaya ya Ruangwa Somoe Kishoka na Fatuma
Saidi wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuuza samaki wenye vimelea
vya Kipindupindu.
Akizungumzia tukio hilo mganga mfawidhi wa zahanati
ya Mpekenyela Mikidad Mbule anathibitisha kupokea wagonjwa hao,huku
ndugu wa mgonjwa aliyelazwa kutokana na maambukizi
anaelezea hali hiyo ilivyomkuta .
0 comments:
Post a Comment