Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo akimkabidhi funguo za gari
jipya la wagonjwa Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete lililotolewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya shughuli
ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.Tukio hilo
lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akipokea na kuangalia
nyaraka za gari hilo la kubebea wagonjwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ikulu Peter
Ilomo.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada
ya kukabidhiwa gari la kubebea Wagonjwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwasha gari jipya la
Wagonjwa lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya
Chalinze.
Sehemu ya Ndani ya gari hilo kama inavyoonekana .
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiendesha gari hilo la
wagonjwa lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya
Chalinze.
Gari jipya la Wagonjwa lililotolewa na Mheshimiwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Hospitali ya
Wilaya ya Chalinze kama linavyoonekana kwa nyuma.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akifurahia mara baada
ya kukabidhiwa Gari hilo la Wagonjwa.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada
ya kukabidhiwa gari na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es
Salaam. Wengine katika picha ni Afisa Usafirishaji wa Ikulu Athuman
Natepe wakwanza kushoto, Mwenyekiti wa Wilaya ya Chalinze Said Omar Zikatimu
wapili kutoka kulia na Dkt. Nasoro Ally Matuzya wakwanza kulia.
Picha na IKULU.
0 comments:
Post a Comment