Aliyekuwa Nahodha na kisha kocha wa timu ya taifa ya
Ujerumani iliyotwaa kombe la dunia Franz Beckenbauer ametajwa katika orodha ya
watuhumiwa 6 wanaoshukiwa kutoa hongo kununua kombe la dunia la mwaka wa 2006
huko Ujerumani.
Kamati ya maadili ya FIFA imetoa orodha wa watu 6
waliongoza kampeini hiyo ya kutwaa uwenyeji wa kombe la dunia.
Shirikisho la soka la Ujerumani lilipasua mbarika
lilipofichua ripoti ya upelelezi ambayo ilimpelekea Nahodha huyo wa zamani wa
timu ya taifa ya Ujerumani kukiri kuwa alifanya makosa wakati wa kuwania zabuni
ya wenyeji wa kombe hilo la dunia.
Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita, Beckenbauer, 70,
aliomba msamaha kwa hatua na kauli alizotoa wakati wa kuwania uwenyeji wa
mashindano hayo.
Ujerumani wakati huo iliishinda Afrika Kusini kwa
kura moja pekee.
Ujerumani ilipata kura 12 dhidi ya 11 za Afrika
Kusini katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 2000.
Orodha kamili
Franz Beckenbauer
Wolfgang Niersbach
Helmut Sandrock
Theo Zwanziger
Horst Schmidt
Stefan Hans.
Jarida la upekuzi la Ujerumani, Der Spiegel mwaka
uliopita liliripoti kuwa waandalizi wa kombe hilo walitenga Euro milioni 6.7
kununua uwenyeji wa mashindano hayo.
Beckenbauer, Zwanziger, Schmidt na Hans
awanachunguzwa kwa makosa ya kutoa hongo ilikuwashawishi wajumbe waipigie
Ujerumani kura pamoja na kutoa zabuni kadhaa kwa wajumbe fulani.
Kwa upande wao Niersbach na Sandrock wanachunguzwa
kwa kosa la kushindwa kuripoti ukiukwaji wa kanuni na maadili ya FIFA.
Beckenbauer aliiongoza kikosi cha taifa cha West
Germany wakati huo kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1974.
Aidha aliifunza timu hiyo miaka 16 baadaye
ilipoibuka mabingwa wa dunia nchini Italia.
Amewahi pia kuifunza timu za Marseille na Bayern
Munich, ambako anaihumia kama rais.
0 comments:
Post a Comment