Marekani
imewaonya raia wake walio Ulaya na wanaopanga kuzuru bara hilo kuhusu uwezekano
wa kutokea kwa mashambulio mengine ya kigaidi.
Tahadhari
hiyo imetolewa baada ya mashambulio kuua watu 34 katika mji wa Brussels
Jumanne.
Wizaya
ya mashauri ya kigeni ya Marekani imesema makundi ya kigaidi huenda
yakatekeleza mashambulio karibuni.
“Makundi
ya kigaidi yanaendelea kupanga mashambulio ya kuteketelezwa karibuni kote
Ulaya, yakilenga hafla za michezo, maeneo ya kitalii, migahawa na uchukuzi,”
taarifa ya wizara hiyo ilisema.
Raia wa
Marekani wanaozuru Ulaya wametakiwa kuwa macho zaidi maeneo yenye watu wengi au
wanapotumia mifumo ya uchukuzi wakati wa sikukuu ya Pasaka.
Miji
mingi Marekani imeimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege na vituo vya treni
na mabasi.
Serikali
hata hivyo imesema bado haina habari za uhakika kuhusu uwezekano wa kutokea kwa
mashambulio Marekani.
Kundi
linalojiita Islamic State (IS) limedai kuhusika katika mashambulio Brussels.
Taarifa
iliyopakiwa mtandaoni na kundi hilo ilisema maeneo hayo yaliyoshambuliwa
“yaliteuliwa kwa umakinifu mkubwa” na kuonya kuwa kutatokea mabaya zaidi kwa
mataifa yanayopinga kundi la Islamic State.
0 comments:
Post a Comment