Mpango huo kwa jina Victoria Derbyshire uliandamana
na nahodha wa kikosi cha timu ya wanawake wa Arsenal Alex Scot ambaye alifanya
mazoezi na watoto hao.
Arsenal wana matumaini kwamba mradi huo utawasaidia
watoto walio katika hali mbaya kuona furaha inayosababishwa na soka.
Esra ambaye sio jina lake rasmi alitoroka karibu na
mji mkuu wa Iraq,Baghdad wakati vita hivyo vilipotokea katika maeneo aliyokuwa
akiishi.
Aliiwacha nyumba kubwa pamoja na bustani ambayo
alikuwa akiangalia yeye na babaake na sasa anaishi katika kambi ya Alwand One
huko Kurdistan,kaskazini mwa Iraq ambayo ni makao ya zaidi ya watu 6000.
''Tumelazimika kuishi kwa kuwa mabomu na milipuko
imekuwa ikitokea na tuliogopa kwamba huenda moja likalenga nyumba yetu''.
''Roketi zilikuwa zikirushwa kwa hivyo tukalazimika
kuondoka kwa haraka.Niliwaaga rafiki zangu wawili'',wengine sikuwaona,alisema
mtoto huyo wa miaka 12.
''Mara ya kwanza nilichanganyikiwa,sikujua vile
ningeondoka nyumbani kwangu na kusafiri hadi hapa,lakini ni saa chache kutoka
mahali vita vilikuwa vikiendelea''.
Katika eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa islamic
State.Tangu Januari 2014,mapigano yamewaacha zaidi ya watu milioni tatu kuwacha
makao yao nchini humo na nusu yake ni watoto.
Na alipoulizwa ni nini kizuri kuhusu kambi hiyo,Esra
alijibu:Shule na uwanja huo wa Soka.
Alex ambaye ameichezea timu ya soka ya Uingereza
anasema kuwa ijapokuwa hawezi kufananisha hali yake na ilivyo sasa,soka
ilimsaidia wakati alipokuwa akikuwa.
Viwanja hivyo vilivyo na nyasi za kijani vinatoa
mandhari nzuri ya rangi katika eneo lililojaa vumbi na kuwapatia watoto hao
eneo salama la kucheza.
Kufikia sasa watoto 2500 wamepata fursa ya kucheza
katika viwanja hivyo.
Huku Alex akiwafunza na kucheza na wasichana,
wavulana wanaonekana wakiangalia katika upande mwengine wenye uwa.
0 comments:
Post a Comment