Bunge la Kenya limeanza mikakati ya kunusuru taifa
hilo kutokana na tuhuma za wanaridha wake kuhusishwa na madai ya utumiaji wa
dawa za kututumua Misilu.
Kamati maalum ya bunge iliyoundwa kujadili suala hilo
ikiongozwa na aliyekuwa Bingwa wa mbio za Boston Marathon mwaka 2012 na
aliye pia mbunge wa bunge la 11 kwa sasa Wesley Koriri mbioni kuweka
sheria zitakazosaidia kupambana na utumizi wa dawa kututumua Misuli.
Wanaridha wa Kenya siku za hivi karibuni wamekuwa
wakikabiliwa na madai ya kuhusika kwenye utumiaji wa dawa za kututumua
Misuli wa hivi punde akiwa bingwa mara mbili wa mbio za iaaf mwaka 2010
na mwaka 2012 Emily Chebet.
Bunge la Kenya linasema likombioni kuunda mamlaka
itakayotwikwa majukumu ya kuchunguza visa vya utumiaji wa dawa hizo ikiangaziwa
kuwa kenya katika upembe wa bara afrika imekuwa kilele kwa mashindano ya
riadha.
0 comments:
Post a Comment