Kipa wa Southampton Fraser Forster ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari Ligi Kuu Uingereza.
Muingereza huyo alikaa muda mrefu nje kutokana na majeruhi na kurudi Januari na kuichezea klabu yake mechi sita bila kufungwa, mechi dhidi ya Arsenal, West Ham na Swansea, na kujinyakulia alama saba Februari.
Forster alikuwa mlinda pekee kutofungwa mechi sita, akiwapiku washambuliaji Harry Kane na Jamie Vardy, viungo Willian na Christian Erikse na mlinda mlango Robert Huth katika tuzo hiyo.
0 comments:
Post a Comment