Serikali ya Kenya inaendelea na juhudi za kupambana
na ufisadi. Rais Uhuru Kenyatta anaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha
serikali yake inakuwa safi ikiwa ni pamoja na kuwaondoa maofisa wa serikali
waliothitibitika kupokea rushwa, licha ya kukabiliwa na changamoto kubwa.
Hivi karibuni alipokuwa ziarani nchini Israel, Rais
Kenyatta alisema licha ya Kenya kujaliwa kuwa nchi nzuri kuliko hata nchi
zilizoendelea, watu wake bado wanaishi maisha magumu kutokana na ufisadi.


0 comments:
Post a Comment