Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
nchini Sudan Kusini Bibi Ellen Margrethe Loj amerudia msimamo wa Umoja huo wa
kuendelea kuwalinda raia nchini Sudan Kusini.
Bibi Margrethe ametoa wito kwa wadau wote nchini
humo kujiepusha na vitendo au kauli zinazoweza kuchochea migogoro, na kuheshimu
kanuni za Umoja wa Mataifa kama vile kutokuwa na silaha kwenye vituo vya Umoja
huo.
Mwakilishi huyo aliyasema hayo wakati akitembelea
eneo la Malakal kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kutathmini hali ilivyo na
kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa kijamii.
Watu wasiopungua 7 waliuawa mwezi uliopita na wengi
kujeruhiwa wakati watu wasiojulikana waliposhambulia kituo cha Umoja wa Mataifa
cha Malakal. Kituo hicho cha Malakal kinahifadhi raia 50,000 ambao wamekimbia
makazi yao kutokana na vita.


0 comments:
Post a Comment