Miongoni mwa wabunge
hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,Mh.Victor
Mwambalaswa Mbunge wa Lupa,Sadick Murad Mbunge wa Mvomero na Kangi Lugola
Mbunge wa Mwibara.
Wabunge hao sasa
wanakamilisha taratibu za dhamana kwa kila mmoja kulipa shilingi Million 5 na
watakua nje hadi April 15 kesi yao itakapo sikilizwa tena.
Hata hivyo kwa siku
kadhaa za nyuma vuguvugu lilitanda juu ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hali
iliyo lazimu kujiuzulu kwa Baadhi ya wabunge.
Kutokana na shutuma za
Rushwa miongoni mwa wabunge akiwamo Mbunge wa Nzega Mjini na Kiongozi wa chama
cha CCM,aliishtumu Kamati ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya
Wajumbe walipokea rushwa na kuchukua uamuzi wa kuungana na Mh.Zitto
Kabwe,kumuandikia barua Spika wa Bunge ya kujiuzulu na kumtaka achunguze na kuchukua hatua.
0 comments:
Post a Comment