Chama cha kandanda nchini Zimbabwe (Zifa) kimemtimua
mwanakamati Edzai Kasinauyo kutokana na madai kuwa alipanga matokeo ya mechi.
Bwana Kasinauyo analaumiwa kwa kushiriki katika
kupanga mechi wakati wa michuono ya nchi hiyo ya kufuzu kwa mashindano ya taifa
bingwa barani Afrika na Swaziland tarehe 25 mwezi Machi.
Taarifa kutoka (Zifa) zilisema kuwa uchunguzi
unaendelea. Kasinauyo mwenye umri wa miaka 40 amekana madai hayo.
Yeye ni mchezaji wa zamani wa kiungo cha kati na
aliwakilisha nchi yake katika mashindano wa kuwania kombe la taifa bingwa
barani Afrika mwaka 2006.
Alichaguliwa kwenye kamati kuu ya Zifa mwezi
Disemba.


0 comments:
Post a Comment