Wataalam huru wa Umoja wa Mataifa wamesema kuna kazi
kubwa ya kufanya nchini Burundi kuhusu haki za binadamu nchini Burundi.
Mmoja wa wataalam Pablo de Greiff amesema katika
wiki ya kwanza ya mwezi huu wamekutana na makundi mbalimbali wakiwemo maofisa
wa serikali, makundi ya kijamii, viongozi wa kidini, mashahidi na waathiriwa.Bw
Greiff pia amepongeza makubaliano ya Arusha ya mwaka 2000 kuhusu amani na kuundwa
kwa tume ya maridhiano nchini Burundi.
Wataalam hao wanasema takwimu zinaonesha kuwa zaidi
ya watu 400 wameuawa nchini humo tangu kuzuka kwa mgogoro uliosababishwa na
Rais Pierre Nkurunziza aliyetangaza kuwania urais kwa awamu nyingine.


0 comments:
Post a Comment