Ofisi ya mkuu wa sheria nchini Uswisi imethibitisha
kuwa utawala nchini Ufaransa umevamia ofisi za shirikisho la kandanda mjini
paris.
Uvamizi huo wa siku ya Jumanne una uhusiano na
uchunguzi unaoendeshwa na uswisi kwa mkuu wa shirikisho la kandanda duniani
FIFA Sepp Blatter.
Maafisa hao walichukua stakabadhi zinazohusiana na
malipo ya dola milioni mbili yaliyofanywa na bwana Blatter kwa mkuu wa
shirikisho la kandanda barani ulaya Michel Platini.


0 comments:
Post a Comment