JESHI la polisi mkoani Ruvuma, linamsaka askari wake
wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mwenye namba F,5425 PC Emmanuel Nyagol (35)
anayedaiwa kutoroka kwa tuhuma za kugushi vyeti wakati akijiunga na jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji alisema askari huyo
alitoroka Machi 16, mwaka huu .
Alisema inawezekana Nyagol amefikia uamuzi huo baada
ya kuwapo tuhuma za kujiunga na jeshi hilo kwa kutumia vyeti vya kughushi jambo ambalo ni kinyume
cha taratibu za nchi.
Alisema
askari huyo aliajiriwa Aprili 28, mwaka 2003 na kupangiwa kituo cha kazi
mkoani Ruvuma, baada ya kuhitimu mafunzo
mkoani Kilimanjaro.
Alisema askari huyo ametoroka na vitu vyake vya
binafsi, kwani sare na vitambulisho
vyote ameviacha. Alisema jeshi hilo, linaendelea na msako dhidi ya PC Nyagol.
0 comments:
Post a Comment