Umoja wa wanawake wa makanisa ya kikirsto Tanzania
(CCT) katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametoa tamko la pamoja
kulaani biashara haramu ya kusafirisha binadamu ndani na nje ya nchi
huku wakiitaka serikali kuchunguza chanzo cha biashara hiyo
na kuwachukulia hatua kali za kisheriri watakaobainika kuhusika na
biashara hiyo.
kauli hiyo imetolewa katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kanisa katoliki Parokia ya mtakatifu Theresia Segese Kahama huku wakidai kuwa waathirika wa kubwa wa biashara hiyo ni wanawake na watoto wakike wanaorubuniwa na kuuzwa kwa watu wasio na malengo mazuri.

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa kinamama
wa CCT kahama Bi. Laurensia Gervas amesema mtandao wa wafanya biashara haramu
ya binadamu imeanza kuota mizizi katika maeneo ya vijijini ambapo
wanazirubuni familia masikini na watu wanaoishi katika mazingira magumu na
kuwachukua watoto wakike kuwauza nje ya nchi.
Bi.Ester Shija ni mlezi wa wanawake kata ya Segese
wilayani Kahama Shinyanga amewaasa wanawake wote nchini kulea familia zao kwa
kuzingatia maadili ya upendo na kuweka misingi mizuri ya malezi huku
akiwataka kuacha kutoa lugha chafu kwa wanaume hali ambayo inachangia
kusanbaratisha ndoa na kusababisha mateso kwa watoto wadogo.

0 comments:
Post a Comment