Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala
Bora,ANGELA KAIRUKI ametoa siku moja kwa
mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na mkoa kwa jumla kutoa maelezo
ya matumizi ya shilingi BILIONI 2.46 zilizotolewa na serikali katika mwaka wa
fedha 2014/2015 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa nyumba za walimu, vyoo na
usimamizi .
Ametoa maagizo hayo baada ya kamati ya bunge ya
utawala bora na serikali za mitaa kutembelea shule ya sekondari kirugu kata ya
majengo mjini Kigoma na kukagua baadhi
ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF awamu
ya pili ambapo ilibainika kuwa shule hiyo haina nyumba za walimu, jingo la
utawala, umeme na vyoo havitoshelezi.
Amesema hali hiyo inaonyesha jinsi fedha
zilizotolewa na serikali hazikutumika kwa malengo yaliyokusudiwa katika mkoa wa
Kigoma na kutaka taarifa hiyo iwasilishwe haraka kwa Waziri wa TAMISEMI -
GEORGE SIMBACHAWENE
0 comments:
Post a Comment