Waziri George Simbachawene ametoa agizo kuwa uchaguzi wa
Meya wa jiji la Dar es Salaam ufanyike kabla ya Machi 25 Mwaka huu.
Agizo hilo la waziri Simbachawene limevitaka pia vyama
vinavyoshiriki uchaguzi wa Meya kuheshimu Democrasia.
Katika hatua nyingine Chama cha CCM kimewatupia lawama
wakurugenzi wa Manispaa na jiji kwamba kushindikana kufanyika kwa uchaguzi wa
Meya wa Jiji la Dar es Salaam wao ndio chanzo na kiini cha tatizo kutokana na
kushindwa kuitafsiri sheria vyema.


0 comments:
Post a Comment