Taharuki kubwa imetanda leo baada ya kutokea ajali
iliyohusisha magari matatu na kupoteza maisha ya watu wa tatu na wengine 19
kujeruhiwa huku wengine hali zao zikielezwa kuwa Mbaya.
Mapema sakumi na moja za asubuhi kilisikika kishindo
kikubwa barabarani mithili ya bunduki hali iliyolazimu raia kujitokeza
kushuhudia hicho kishindo kilikuwa cha nini ndipo wakakuta ajali iliyo husisha
magari hayo matatu.
Kwa mujibu wa Mashuhuda walidai kuwa watu
waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo huenda wakazidi 10 kutokana na jinsi
walivyokuwa wakiokoa waliona na hata kushuhudia hali mbaya zao zilizokuwa
hazina matumaini ya uhai na wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya na gari likiwa
limeharibika vibayaya.
Polisi wa ilala walithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kueleza kuwa Chanzo cha ajaki ni Lori la Mchanga kuligonga basi
la abiria aina ya DCM kwanyuma ndipo likayumba likapoteza muelekeo na kujikuta
likimshinda dereva na kuruka upande wa pili wa bara bara ndipo likakutana uso
kwa uso na Lori lililokuwa limebeba Ng’ombe likipeleka machinjio ya Vingunguti
na hivyo kutokea kwa ajali.
Basi la Abiria lilikuwa likitokea Gongo la Mboto
Ubungo DCM T 629 CRT huku likiwa linaongozana na Lori lamchanga T 277 DAU
lililokuwa limeligonga kwa nyuma(Ubavuni) ndipo hapo sasa derweva wa DCM gari
ikamshinda nguvu na likavuka upande wa pili likakutana na Lori T 109 DDX ambalo
nalo lilikuwa lipo mwendo wa kasi likiwahi kupeleka Ng’ombe mnadani vingunguti
likitokea njia ya Ubungo.
Mashuhuda waliokuwa hapo eneo la tukio ndio
waliokuwa wakwanza kutoa msaada kwa majeruhi na na waliopoteza maisha
kusaidiana na polisi kuwapandisha kwenye gari kusudi wawahishwe Hospitalini.
Mashuhuda waliokutwa na kamera yetu ya Tambarare
Halisi waliduwaa kuangalia ajali hiyo huku wengine wakiishiwa hata nguvu kwa
kuona ndugu na jamaa zao wakiwa katika hali mbaya baada ya ajali.
Wamesema kunahaja kwa madereva kuwa makini sana huku
wakitupia lawama Lori la mchanga lililoonekana kutaka kulipita basi la abiria
kusudi liwahi nahivyo kujikuta safari hiyo ikiishia Tabata Matumbi baada ya
ajali kutokea.
Licha ya Polisi kufika eneo hilo wamesem,a kuwa kuna
haja ya eneo hilo kuwekwa matuta kwani ajali zimekuwa ninyingi zikitokea eneo hilo
si mchana wala usiku hivyo ipo haja uangaliwe utaratibu.
Hata hivyo kutokana na ajali hiyo foleni ilichukua
takribani saa tatu ndipo msaada wa kuondolewa kwa gari hizo zilizopata ajali
zikaanza eneo hilo.
Waliopoteza Maisha na Majeruhi inaelezwa wamehifadhiwa
hospitali ya Muhimbili na wengine Amana jijini Dar es Salaam.
Tutaendelea kuwafahamisha kitakacho jiri zaidi.
ubavuni lilokuwa linatoka Buguruni kuelekea Ubungo
na kisha basi hilo kupoteza muelekeo wa safari na kuruka upande wa pili wa
barabara na kugongwa tena na lori lingine aina ya SCANIA lilokuwa limebeban
ng’ombe waliokuwa wanapelekwa Machinjioni.Polisi wamethibitisha hilo.


0 comments:
Post a Comment